Friday, July 25, 2014

Kuwepo kwa migogoro ya ardhi na vitendo vya imani za kishirikina ni moja ya sababu zinazoyagharimu maisha ya wanawake vikongwe kuuwawa kwa kukatwa mapanga  mkoani simiyu ,hivyo jeshi la polisi limekemea na kuitaka jamii kuanzisha daftari la wageni kwa kila kijiji ili kuwabaini wanaoingia na kutoka.
Akizungumza na  viongozi na wananchi wa kata ya kiloleli kamanda wa polisi wa mkoa wa simiyu kamishina msaidizi mwandamizi charles mkumbo amesema kuwa vitendo vya mauaji ya vikongwe vinavvyohusishwa na imani za kishirikina ,kamwe jeshi halitawavumilia wanaoendesha mauaji hayo .
Mkumbo amewataka wananchi kuondokana na na fikra hizo potofu zinazoyagharimu maisha ya akinamama na kuviagiza vijiji vyote vya kata ya kaloleli wilayani busega kuanzisha daftari la wageni ,wanaoingia na kutoka ,hali ambayo itasaidia kuwabaini wahalifu na hatimaye kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande wao wakazi wa kata ya kiloleli wanaelezea namna ushirikina unavyomaliza nguvu kazi ,huku wengine wakiahidi  kuyafanyia kazi maagizo yaliyotolewa na kamanda wa polisi ya ulinzi shirikishi.
Katika hatua nyingine mkumbo amewaonya wanasiasa katika kata hiyo wanaowagawa wananchi katika kipindi hiki na kuwataka kufanya siasa za kistaarabu na sio kuwatisha wananchi .

No comments:

Post a Comment