Kuwepo kwa
migogoro ya ardhi na vitendo vya imani za kishirikina ni moja ya sababu
zinazoyagharimu maisha ya wanawake vikongwe kuuwawa kwa kukatwa mapanga mkoani simiyu ,hivyo jeshi la polisi
limekemea na kuitaka jamii kuanzisha daftari la wageni kwa kila kijiji ili
kuwabaini wanaoingia na kutoka.
Akizungumza
na viongozi na wananchi wa kata ya kiloleli
kamanda wa polisi wa mkoa wa simiyu kamishina msaidizi mwandamizi charles
mkumbo amesema kuwa vitendo vya mauaji ya vikongwe vinavvyohusishwa na imani za
kishirikina ,kamwe jeshi halitawavumilia wanaoendesha mauaji hayo .
Mkumbo
amewataka wananchi kuondokana na na fikra hizo potofu zinazoyagharimu maisha ya
akinamama na kuviagiza vijiji vyote vya kata ya kaloleli wilayani busega
kuanzisha daftari la wageni ,wanaoingia na kutoka ,hali ambayo itasaidia
kuwabaini wahalifu na hatimaye kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande
wao wakazi wa kata ya kiloleli wanaelezea namna ushirikina unavyomaliza nguvu
kazi ,huku wengine wakiahidi kuyafanyia
kazi maagizo yaliyotolewa na kamanda wa polisi ya ulinzi shirikishi.
Katika hatua
nyingine mkumbo amewaonya wanasiasa katika kata hiyo wanaowagawa wananchi
katika kipindi hiki na kuwataka kufanya siasa za kistaarabu na sio kuwatisha
wananchi .
No comments:
Post a Comment