Friday, July 25, 2014

Waandishi wa habari  hawana budi kutumia kalamu zao katika kuwafichua watu wanaondelea kuwafanyia ukatili wa kijinsia watoto wa kike na wanawake kwa kuwashushia vipigo na kuwasababishia ulemavu wa  maisha.
Rai hiyo ilitolewa  jijini mwanza na mkurugenzi wa UTPC Bw. Abubakari karsan wakati akifungua mafunzo ya waandishi wa habari kutoka mikoa mitano ya kanda ya ziwa ,ambayo yameandaliwa na chama cha waandishi wa habari wanawake tanzania  Tamwa,ikiwa ni mikakati ya kupambana na ukatili wa kijinsia hapa nchini.
Karsan Alisema kuwa dhima ya vyombo vya habari  katika vita  dhidi ya uovu wa ukatili wa kijinsia  ukiachwa bila kushughulikiwa unaweza kuvunja mshikamano wa kijamii hali ambayo inaweza kuleta mparanganyiko wa taifa, na hivyo kuwaomba waandishi wa habari  kufichua  vitendo hivyo kwa kutumia kalamu zao.
Alisema  wanawake wanaathirika  kutokana na  fikra  kengefu  inayojengwa na jamii kwamba  mwanamke ni kiumbe dhaifu anayestahili kusaidiwa ,huku baadhi wakifungiwa ndani  na kunyimwa fursa za kielimu  ususaniwatoto wa kike  .

Kwa upande wake mkurugenzi wa tamwa valerie msoka aliwataka  waandishi wa habari wanawake kutokakata tamaa  katika mapambano dhidi ya unyanyasaji  bali wakubaliane na changamoto zilizopo.

No comments:

Post a Comment